Mgomo wa Benki ya NMB nchini Tanzania
24 Septemba 2008Matangazo
Wafanyakazi hao waliitisha mgomo huo kama njia ya kushinikiza kutekelezwa kwa matakwa yao ambayo ni kusainiwa kwa makubaliano ya kulipwa asilimia tano ya hisa pamoja na fedha za mfuko wa kujikopesha. Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Ernest Mwaipopo aliwataka wafanyakazi hao kurejea kazini kuanzia saa mbili asubuhi leo hii.
Ili kufahamu ni vipi amri hiyo imetekelezwa Aboubakary Liongo alizungumza na mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi hao, Joseph Masana.