Mgogoro wa Msikiti Mwekundu nchini Pakistan. | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mgogoro wa Msikiti Mwekundu nchini Pakistan.

Katika mgogoro wa msikiti mwekundu mjini Islamabad Pakistan , kiongozi wa msikiti huo sheikh Abdul Rashid Ghazi amesema yupo tayari kufanya mazungumzo kwa kutumia njia ya kipaza sauti .

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan

Waziri Mkuu bwana Shaukat Azizi amesema kuwa sheikh huyo ataruhusiwa kuonana na mama yake ikiwa atasalimu amri. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wam rais

Rais Pervez Musharraf kumteua aliekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo kusuluhisha katika mgogoro huo ambapo watu 24 tayari wameshauawa tokea uanze.

Waziri mkuu wa Pakistan bwana Shukat Azizi amefahamisha kwamba serikali itamruhusu sheikh Abdul Rashidi Ghazi kuwekwa chini ulinzi nyumbani alipo mama yake mgonjwa ikiwa atasalimu amri na kuwaachia wanawake na watoto anaowashikilia ndani ya msikiti.

Leo ni siku ya saba tokea waislamu hao wenye itikadi kali wamekuwa wanawashikilia wanawake na watoto hao ndani ya msikiti huo katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad.

AM.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com