Mfumo wa elimu wa Ujerumani umefeli | Magazetini | DW | 19.09.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mfumo wa elimu wa Ujerumani umefeli

Kuwachuja mapema wanafunzi ndio chanzo cha kasoro za mfumo wa elimu

Mfumo wa elimu nchini Ujerumani ndio mada iliyochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Licha ya juhudi zote za mageuzi,mfumo wa elimu wa Ujerumani umefeli kwa mara nyengine tena ukilinganishwa na mfumo wa elimu wa kimataifa.Wasomi wachache,uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi,kiwango cha chini cha uwekezaji na ukosefu wa usawa- ni miongoni mwa kasoro zilizoorodheshwa na shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD-katika uchunguzi wake wa hivi karibuni.Waziri wa elimu wa serikali kuu ya Ujerumani Anette Schavan wa kutoka chama cha CDU anakumbwa na lawama tuu na ubishi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani .

Gazeti la mjini Cologne-KÖLNER STADT-ANZEIGER linaonya dhidi ya kupuuzwa taftishi ya shirtika la OECD.Gazeti linaendelea kuandika:

Wanasiasa wamekua kila kwa mara, katika miaka ya nyuma wakijarivu kuufanyia marekebisho mfumo wa elimu .Matokeo ya maana lakini hayajapatikana.Wasomi ni haba nchini Ujerumani.Hali hii inatokana zaidi na ule ukweli kwamba ufanisi katika masomo mara nyingi unategemea tabaka ya kijamii.Ikitaka kushindana katika daraja ya kimataifa Ujerumani haitastahiki kuviachia vivi hivi tuu vipaji vyake.”

Hoja sawa na hizo zimetolewa pia na gazeti mji jirani wa Bonn-GENERAL-ANZEIGER linaloandika:

“ Nchini Ujerumani hasa ndiko ufanisi katika masomo unategemea zaidi tabaka ya jamii, hali ambayo haikutikani katika nchi yoyote ile nyengine.Kwa miaka sasa wanasiasa wamekua wakipitisha hatua zile zile kujibu taftishi kama hizi.Lakini kama Ujerumani haitaufanyia mageuzi ya kina mfumo wake wa elimu, kuhakikisha hali ya usawa kwa wote na kuachana na utaratibu wa kuchuja tangu mwanzo,basi hata zile cheche za mwisho za matumaini ya kua na jamii ya walioelimika, zitatoweka.”

Gazeti la WESTFÄLISCHE ANZEIGER la mjini Hamm halioni matumaini yoyote.Gazeti linaandika:

„Mara tuu baada ya ripoti mpya ya shirika la OECD kutangazwa,mdajala ule ule wa kisiasa ulioshawishiwa kinadharia umepamba moto-kila mmoja anataka kujijenga.Watu wanajisumbua tuu.Hakuna hatua zozote za maana zitakazopitishwa na wahusika.“

Gazeti la TAGESSPIEGEL na mjini Berlin linaandika:

„Itakua shida zaidi kubadilisha mfumo wa elimu katika daraja ya kitaifa,kwasababu elimu inabakia kua jukumu la serikali za majimbo.Kwa hivyo hakuna dalili zozote kama Ujerumani itaweza wenyewe kurekebisha kasoro zilizoko katika mfumo wake wa elimu.Panahitajika wasomi kutoka nje.Ukweli huo lakini hatutaki kutambua.“

 • Tarehe 19.09.2007
 • Mwandishi Scheithauer / Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHRn
 • Tarehe 19.09.2007
 • Mwandishi Scheithauer / Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHRn