MEXICO CITY : Tetemeko la ardhi lapiga Mexico | Habari za Ulimwengu | DW | 13.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MEXICO CITY : Tetemeko la ardhi lapiga Mexico

Tetemeko la ardhi lenye nguvu la kipimo cha 6. 2 limetingisha mwambao wa kati nchini Mexico.

Uchunguzi wa Giolojia wa Marekani umesema kwamba tetemeko hilo limepiga maili 60 kaskazini mwa Acapulco katika mwambao wa Pasifiki wa nchi hiyo.Watalii kwenye mahoteli wametimka kutoka vyumba vyao wakihofia kuzuka kwa matetemeko mengine madogo madogo ambayo kwa kawaida hufutia baada ya kupiga kwa tetemeko kuu.

Temeko hilo liliweza kuhisiwa katika baadhi ya sehemu za mji mkuu wa Mexico City ambao umeme ulikatika.

Kumekuwa hakuna taarifa juu ya majeruhi au uharibifu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com