1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mexico

Mexico ni nchi ambako ukwasi, umaskini, uzuri wa asili na uozo wa mjini vinakutana. Ina uchumi wa pili kwa ukubwa katika bara la Amerika Kusini na ni muuzaji mkubwa wa mafuta.

Lakini mafanikio yanaendelea kuwa ndoto kwa Wamexico wengi na pengo la kiuchumi na kijamii linabakia kuwa kubwa. Wamexico wengi wamevuka mpaka wa kilomita 3000 kati ya nchi yao na Marekani kutafuta ajira nchini Marekani, lakini katika miaka ya karibuni Wamexico wengi wamevuka mpaka kurudi nyumbani kuliko waliohamia Marekani. Mamia kwa maelfu ya watu wameuawa katika vurugu zinazohusiana na magenge ya madawa katika muongo uliopita. Makundi yenye nguvu yanadhibiti biashara ya usafirishaji madawa kutoka Amerika Kusini kwenda Marekani. Vikosi vya usalama vilivyoamriwa kuyashughulikia vimelaumiwa kwa kutumia vibaya mamlaka yao na kuchukuwa hatua bila kuwajibishwa.

Onesha makala zaidi