Merkel akataa pendekezo la Sarkozy | Habari za Ulimwengu | DW | 06.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Merkel akataa pendekezo la Sarkozy

BERLIN

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amelikataa pendekezo la Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alilotowa nchini Algeria la kuwepo kwa umoja wa nchi za Mediterranean .

Merkel amesema ana hofu mpango huo unaweza kutishia Umoja wa Ulaya.Sarkozy mara ya kwanza aliwasilisha mpango wa kuwepo kwa umoja huo hapo mwezi wa Mei wakati alipopendekeza kwamba nchi zote zenye kupakana na bahari ya Mediterranean ziwe na mkutano wa viongozi chini ya urais wa kupokezana.

Merkel na Sarkozy wanatazamiwa kukutana mjini Paris leo hii kwa mazungumzo yasio rasmi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com