1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

G7 yatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita Ukraine

13 Novemba 2025

Katika mkutano uliofanyika nchini Canada, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 wametoa wito wa dharura wa kusitishwa kwa vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/53WDI
G7- Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani 2025 | Niagara-on-the-Lake
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 katika picha ya pamojaPicha: Mandel Ngan/AFP

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 wametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

Katika tamko la pamoja, mawaziri kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, na Marekani wameeleza kuunga mkono kwa dhati uhuru wa Ukraine, huku wakionyesha wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchini Sudan.

Mazungumzo hayo yalifanyika karibu na maporomoko maarufu ya maji ya Niagara Falls, ambapo viongozi hao walijadili mikakati ya kuimarisha ufadhili kwa juhudi za Ukraine kupambana dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Miongoni mwa ajenda kuu zilizojadiliwa ni pendekezo la "kutumia zaidi mali za serikali ya Urusi zilizozuiliwa” katika nchi mbalimbali za G7 — mkakati tata unaoendelea kujadiliwa kwa kina ndani ya Umoja wa Ulaya.