Malkia wa Uholanzi aruhusu serikali kuundwa.
8 Oktoba 2010Matangazo
Serikali hiyo itaundwa kwa kushirikiana na chama cha Christian Democrats na pia kuungwa mkono bungeni katika masuala fulani, na chama cha mwanasiasa mbaguzi anayeupinga uislamu, cha Uhuru, Geert Wilders.
Kulingana na makubaliano hayo yaliyofikiwa wiki moja iliyopita, chama cha Wilders kitakuwemo katika baraza la mawaziri litakaloundwa, ambalo malkia amemtaka bwana Rutte kulishughulikia haraka iwezekanavyo.
Uholanzi imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu muungano uliokuwa madarakani, ambao ulikuwa ukiongozwa na Waziri mkuu Jan Peter Balkenende kuvunjika, Februari mwaka huu.
Rutte anatarajiwa kuongoza serikali ya kwanza ya wachache tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
Mwandishi: Halima Nyanza (zr)
Mhariri: Josephat Charo