1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

The Hague

Mji wa The Hague, ambao unajulikana pia kama "Mji wa Kifalme pembezoni mwa Bahari", ndiyo mji wa tatu kwa ukubwa nchini Uholanzi. Serikali ya Uholanzi na bunge vina makao yake mjini The Hague.

Mbuga, majumba ya kifahari na mitaa mikubwa -Mji wa The Hague (Den Haag katika Kidachi), wenye wakaazi zaidi ya 500,000 ndiyo mji mkuu wa mkoa wa South Holland. Ndiyo mji wa tatu kwa ukubwa baada ya Amsterdam - mji mkuu wa Uholanzi - na Rotterdam. Mji huo mara kadhaa hupamba vichwa vya habari za kimataifa kutokana na ukweli kwamba makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC yanakutikana huko. Utajo wa kwanza wa mji wa The Hague katika historia ulikuwa katika mwaka 1230, wakati nyumba ya wageni ya wawindaji ilipojengwa huko na lodi Floris wa nne, na baadae ikajengwa kama kasri. Jina la The Hague, linatokana na neno la 'hedge' kama ua wa jengo hilo. Na hapa utakuta mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu The Hague.

Onesha makala zaidi