MAKKA: Siku kuu ya Eid al- Fitr yasherehekewa | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAKKA: Siku kuu ya Eid al- Fitr yasherehekewa

Leo ni siku kuu ya Idd el Fitr, siku kuu inayoanza baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu walikuwa wakifunga kwa kujizuwia kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jua linapotua, kutenda mema na kujiepusha na aina yote ya maasi kwa mwezi wote huo.

Siku kuu hii huadhimishwa kwa kutegemea kuonekana kwa mwezi. Baadhi ya nchi kama Saudi Arabia, mataifa ya kifalme ya Ghuba, Uganda, Rwanda na Burundi wanasherehekea Idd el Fitr leo hii. Wengine kama vile nchini Tanzania na Kenya watasherehekea kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com