Luxembourg: Waziri mkuu wa Luxembourg Jean Claude Juncker anahisi duru mpya ya majadiliano | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2003
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Luxembourg: Waziri mkuu wa Luxembourg Jean Claude Juncker anahisi duru mpya ya majadiliano

kuhusu katiba ya Ulaya haitafanyika kabla ya nusu ya pili ya mwaka ujao.Akihojiwa na gazeti la "Financial Times Deutschland" waziri mkuu wa Luxembourg amesema anaamini mazungumzo yataanza upya Uholanzi itakapokabidhiwa zamu ya mwenyekiti wa umoja wa Ulaya.Ameonya dhidi ya mpango ulioshauriwa na waasisi wa Umoja wa Ulaya:Ujerumani,Ufaransa,Italy na nchi tatu za Benelux,yaani Ubeligiji,Uholanzi na Luxembourg wa kushirikiana zaidi hadi katiba mpya itakapopitishwa.Duru ya kwanza ya mazungumzo ya nchi hizo sita huenda ikaitishwa mwezi january au february mwakani.