1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la Lufthansa lasitisha safari za ndege za Tehran

Sylvia Mwehozi
11 Aprili 2024

Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa limesitisha safari za ndege za Tehran kutokana na hali inayoendelea Mashariki ya Kati kutokana na kuwepo na uwezekano wa Iran kufanya mashambulizi ya kulipa kisasi dhidi ya Israel.

https://p.dw.com/p/4edpr
Ndege ya Lufthansa
Ndege ya Airbus A 380 ya LufthansaPicha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/picture alliance

Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa limesitisha safari za ndege za Tehran kutokana na hali inayoendelea Mashariki ya Kati. Eneo hilo lipo katika tahadhari ya uwezekano wa Iran kufanya mashambulizi ya kulipa kisasi kutokana na shambulio la anga la Israel dhidi ya ubalozi wa Tehran nchini Syria.Raisi: Iran italipa kisasi shambulio la ubalozi wetu Syria

Taarifa ya shirika hilo imesema kuwa wanasimamisha safari za ndege za kwenda na kutoka Tehran kutoka Aprili 6 hadi pengine Aprili 11.

Baadhi ya nchi katika kanda hiyo, ikiwemo Marekani zimekuwa katika hali ya tahadhari na kujiandaa kwa mashambulizi yanayoweza kufanywa na Iran tangu Aprili mosi.

Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alisema kuwa Israel lazima iadhibiwe kwa shambulio la Damascus ambalo liliwaua maafisa saba wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi.