1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Jeshi la Ujerumani - Bundeswehr

Bundeswehr ni jeshi la Ujerumani ambalo ni kubwa zaidi barani Ulaya. Bundeswehr linajumuisha jeshi la ardhini, jeshi la majini pamoja na jeshi la angani.

Kufuatia kupunguzwa kwa idadi ya wanajeshi pamoja na kusimamishwa kwa michango mwaka 2011, jeshi hilo lilipungua nguvu na kubaki na wanajeshi 180,000. Tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia Ujerumani imepunguza kutuma wanajeshi wake nje ya nchi. Lakini tokea miaka ya 1990, jeshi hilo limeshiriki katika vita kadhaa duniani. Tangu mwaka 2002 zaidiya wamajeshi 100,000 wameshatumwa nchini Afghanistan.