1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Marekani yajitayarisha na kitisho cha shambulizi la Iran

6 Aprili 2024

Marekani imo katika hali ya juu ya tahadhari ikijitayarisha na uwezekano wa shambulizi kutoka Iran.

https://p.dw.com/p/4eURi
Iran, Teheran | Mazishi ya maafisa wa jeshi waliouwawa kwenye shambulizi linaloaminika kufanywa na Israel dhidi ya ubalozi wa Iran nchini Syria.
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei akiongoza mazishi ya maafisa wa jeshi waliouwawa kwenye shambulizi linaloaminika kufanywa na Israel dhidi ya ubalozi wa Iran nchini Syria. Picha: Iranian Supreme leader's Office/dpa/picture alliance

Shambulizi hilo yumkini litayalenga maslahi ya Washington au Israel kwenye kanda ya Mashariki ya Kati kujibu hujuma iliyofanywa na Israel kwenye jengo la ubalozi wa Iran nchini Syria.

Shirika la Habari la Reuters limeripoti taarifa hizo likimnukuu afisa wa serikali ya Marekani ambaye maelezo yake yamethibitisha ripoti ya kituo cha televisheni cha CNN iliyosema Iran huenda itashambulia mnamo wiki ijayo.

Rais Joe Biden alizungumzia kitisho cha Iran alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, siku ya Alhamisi.

Ndege zinazoaminika kuwa za Israel ziliulenga ubalozi wa Iran mjini Damascus siku ya Jumatatu katika shambulizi lililomuua kamanda mmoja na makuruta kadhaa wa jeshi la Iran.

Viongozi wa serikali mjini Tehran wameapa kuwa watajibu shambulio hilo wakisema Iran inayo haki ya kufanya hivyo.