1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Netanyahu: Tutajibu iwapo Iran itatushambulia

5 Aprili 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametishia kuchukua hatua nzito iwapo Iran itaishambulia nchi yake akisema dola hiyo ya uajemi imekuwa kitisho kwa usalama wa Israel kwa miaka mingi.

https://p.dw.com/p/4eRqd
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Maya Alleruzzo/AP/dpa/picture alliance

Akizungumza kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa mjini Tel Aviv, Netanyahu amesema kitisho hicho cha Iran ambacho ni cha moja kwa moja na pia kupitia makundi inayoyaunga mkono, ndiyo kimeilazimisha Israel kujibu mapigo kwa kuyalenga maslahi ya Tehran na washirika wake.

Amesema Israel itajibu vikali kujilinda iwapo itashambuliwa akiapa kwamba yeyote atayeitakia mabaya nchi hiyo "naye pia atadhurika."

Maafisa wa Israel na Marekani wana wasiwasi mkubwa kwamba Iran inapanga kufanya shambulizi kujibu hujuma inayoaminika kufanywa na Israel dhidi ya jengo lake la ubalozi nchini Syria lililotokea siku ya Jumatatu.

Viongozi wa Iran wamesema "hawatakaa kimya" kufuatia shambulio hilo liliwaua makamanda wake wawili na maafisa kadhaa wa kijeshi.