1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raisi: Iran italipa kisasi shambulio la ubalozi wetu Syria

4 Aprili 2024

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema kwa mara nyingine nchi yake itajibu shambulizi linaloshukiwa kufanywa na ndege za Israeli dhidi ya jengo la ubalozi wa Iran nchini Syria ambalo liliwaua makamanda wa jeshi la Iran.

https://p.dw.com/p/4ePGX
Iran, Tehran | Ebrahim Raisi
Rais wa Iran Ebrahim RaisiPicha: Rouzbeh Fouladi/ZUMA/picture alliance

Kupitia hotuba kwa njia ya televisheni, Raisi ameapa kwamba shambulio hilo "halitakaliwa kimya" na kusisitiza kuwa utawala mjini Tehran utalipa kisasi dhidi ya kile amekitaja kuwa "uhalifu wa kigaidi".

Matamshi sawa na hayo yametolewa pia na kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei. Shambulio hilo la siku ya Jumatatu liliilenga sehemu ya ubalozi wa Iran kwenye mji mkuu wa Syria, Damascus na kuwaua mabrigedia wawili na maafisa wengine wa Kikosi cha Ulinzi wa Mapinduzi cha jeshi la nchi hiyo.

Iran imeituhumu Israel kuwa imefanya shambulio hilo na hata Marekani pia inaamini Israel ilihusika na hujuma hiyo.