1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi mkuu wa Iran aapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel

10 Aprili 2024

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesisitiza leo kuhusu ahadi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel kwa mauaji ya majenerali wa Iran nchini Syria.

https://p.dw.com/p/4ec1t
Iran Teheran | Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Picha: Iranian Supreme Leader's Office/ZUMA Press/picture alliance

Khamenei amesema hayo katika hafla ya kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kusema kuwa shambulio la anga dhidi ya ubalozi wake mdogo nchini Syria mapema mwezi huu lilikuwa kosa dhidi ya kituo cha kidiplomasia kinachochukuliwa kuwa eneo la Iran.

Balozi katika nchi yoyote huchukuliwa kuwa ni sehemu ya nchi inazozimiliki. Wakati Israel inaposhambulia ubalozi wetu, ni kana kwamba imeishambulia nchi yetu. Hii ni kawaida ya kimataifa.

Khamenei ameongeza kuwa utawala huo aliouita mbaya lazima uadhibiwe na kwamba utaadhibiwa.

Kwa kujibu, Israel imesema kuwa vikosi vyake vitaishambulia Iran moja kwa moja ikiwa taifa hilo la Kiarabu litaanzisha mashambulizi dhidi yake.