LONDON:Gordon Brown ateuwa baraza lake la mawaziri | Habari za Ulimwengu | DW | 28.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Gordon Brown ateuwa baraza lake la mawaziri

Waziri mkuu mpya wa Uingereza Gordon Brown ameliteua baraza lake la mawaziri.

David Miliband waziri wa zamani wa Mazingira ndie waziri mpya wa mambo ya nje.

Miliband mwenye umri wa miaka 41 ndie kiongozi wa kwanza mwenye umri wa chini kushikilia wadhfa huo katika kipindi cha miaka 30 nchini Uingereza.

Waziri mkuu wa Uingereza amemteuwa Alistair Darling kuchukuwa wadhfa wa waziri wa fedha, Darling alikuwa waziri wa biashara na viwanda kwa kipindi chote cha miaka kumi cha utawala wa waziri mkuu mstaafu Tony Blair.

Kufuatia kujiuzulu waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza John Reid waziri mkuu Gordon Brown amemteuwa Jacqui Smith mwenye umri wa miaka 44 kuchukuwa wadhfa huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com