Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
Bunge ni chombo cha kiserikali kilicho na jukumu la kutunga sheria, ambacho wawakilishi wake huchagliwa na waanchi.
Katika ukurasa huu tunakukusanyia maudhui mbalimbali zinazohusiana na bajeti.
Tume ya IEBC imetangaza matokeo kutokea maeneo 51 kati ya 290 ya bunge ya uchaguzi wa urais kufikia sasa. Tume hiyo imepewa muda wa hadi tarehe 16 kutangaza matokeo yote.
Tume ya uchaguzi nchini Kenya inaendelea na mchakato wa kutangaza matokeo ya kinyang'anyiro cha urais kutokea maeneo bunge, baada ya kufanyiwa uhakiki na kujumlishwa siku tatu baada ya uchaguzi kufanyika.
China imetangaza kumuwekea vikwazo spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi kufuatia ziara yake ya Taiwan mwanzoni mwa wiki.
Siku moja baada ya Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi, kumaliza ziara yenye utata kisiwani Taiwan, China, ambayo ilikasirishwa sana na ziara hiyo, inaanza mazoezi makubwa kabisa ya kijeshi kuzunguka kisiwa hicho.
Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi ameondoka Taiwan na kusema kwamba yeye na wabunge wengine katika ujumbe wake wameoneesha kuwa hawataacha kujitolea kwao katika kisiwa cha Taiwan kinachojitawala.
Licha ya vitisho kutoka Beijing, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, amewasili Taiwan na kuzungumza na rais na naibu spika wa bunge, huku China ikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho.
Awali China ilitahadharisha kuwa Marekani italipa gharama ikiwa Spika wa Bunge Nancy Pelosi atazuru Taiwan. Wakati huo huo Urusi imesema imefungamana na China, na kuita matarajio ya ziara ya Pelosi kuwa uchokozi mtupu.
Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi amezuru nchini Singapore na kuzungumz na maafisa wa taifa hilo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya bara Asia huku wasiwasi ukitanda wa kutokea mvutano kama atazuru Taiwan.
Mamia ya wafuasi wa kiongozi wa kidini wa Iraq Moqtada al-Sadr walilivamia bunge Jumatano ambapo walionekana wakiimba na kucheza baada ya kuwazidi nguvu maafisa wa usalama.
Wagombea wawili wanaowania nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza wameanza harakati za kusaka kura za wanachama wa chama cha Conservative.
Wabunge nchini Sri Lanka wamemchagua kaimu rais Ranil Wickremesinghe kuwa rais mpya wa nchi hiyo na kutarajia uzoefu wake serikalini utasaidia kuliokoa taifa hilo kutokana na uchumi unaodorora na mzozo wa kisiasa.
Wabunge wa Sri Lanka Jumatano walimchagua waziri mkuu Ranil Wickremesinghe kuwa rais wa nchi hiyo na kuchukua nafasi ya kiongozi aliyeondolewa madarakani Gotabaya Rajapaksa.
Waziri Mkuu Sri Lanka Ranil Wickremesinghe leo ameapishwa kuwa rais wa mpito wa taifa hilo hadi bunge litakapomchagua mrithi wa Gotabaya Rajapaksa, Aliyejiuzulu kufuatia maandamano ya umma.
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameahidi kufanyia kazi mabadiliko ya katiba na sera nyingine muhimu yaliyoanzishwa na mtangulizi wake Shinzo Abe aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumaa iliyopita kwenye mkutano wa siasa.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson atakabiliwa na maswali bungeni Jumatano na baada ya hapo adadisiwe na wakuu wa kamati za bunge huku wadhfa wake wa waziri mkuu ukiwa hatarani.
Aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje wa Israel Yair Lapid leo amechukua nafasi ya Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo na anatarajiwa kuiongoza Israel hadi mwezi Novemba, wakati nchi hiyo ya Mashariki ya kati itakapofanya uchaguzi.