1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Washukiwa 9 wa ugaidi wamekamatwa Uingereza

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCW8

Polisi nchini Uingereza wanawahoji watu 9 waliokamatwa siku ya Jumatano katika mji wa Birmingham,wakishukiwa kupanga njama ya kigaidi ya utekajinyara.Washukiwa hao ambao baadhi kubwa ni wenye asili ya Kipakistani,walikamatwa sehemu mbali mbali za mji wa Birmingham.Inasemekana kuwa washukiwa hao walipanga kumteka nyara mwanajeshi wa Kingereza alie Muislamu na kumkata kichwa na baadae kuonyesha kitendo hicho kwenye mtandao wa Internet.Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imesema,washukiwa hao wamekamatwa kufuatia uchunguzi wa miezi sita uliofanywa na Scotland Yard,polisi wa mji wa Birmingham na vile vile idara ya upelelezi-MI5.