LONDON: Suala la Zimbabwe lijadiliwe Umoja wa Mataifa | Habari za Ulimwengu | DW | 17.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Suala la Zimbabwe lijadiliwe Umoja wa Mataifa

Uingereza inataka suala la Zimbabwe lijadiliwe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Wito huo umetolewa baada ya kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe,Morgan Tsvangirai kutoka hospitali ambako alikuwa akipata matibabu kwa majeraha anayosema kuwa yalisababishwa na polisi waliompiga kikatili.Kiongozi wa chama cha upinzani MDC,amesema ataendelea kumpinga Rais Robert Mugabe.Tsvangirai na wafuasi wa upinzani wapatao darzeni kadhaa walikamatwa siku ya Jumapili,walipokuwa njiani kwenda kuhudhuria mkutano wa kumpinga Mugabe.Serikali imesema, Tsvangirai na kikundi chake waliwapinga polisi waliotaka kuwakamata na vile vile wanafanya kampeni ya ghasia wakitaka kumpindua Mugabe mwenye umri wa miaka 83.Taifa la Zimbabwe ambalo hapo zamani lilikuwa eneo lililozalisha nafaka kwa wingi barani Afrika,sasa chini ya utawala wa Mugabe ni nchi yenye upungufu mkubwa wa chakula na kiwango cha mfumuko wa bei ni kubwa kabisa kote duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com