1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUWAIT:Wafungwa 5 wa Guantanamo wapelekwa nyumbani

4 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEM5

Wakuwaiti 5 waliozuiliwa na Marekani katika jela ya Guantanamo Bay nchini Cuba wamerejeshwa Kuwait ambako watafunguliwa kesi katika mahakama ya nchi yao.Watu hao watano walizuiliwa katika jela ya Guantanamo Bay tangu mapema mwaka 2002 wakishukiwa kuwa ni magaidi.Hali ya afya ya wafungwa 2 inasemekana kuwa ni mbaya sana.Mmoja wao ni miongoni mwa Wakuwaiti watano walioungana na wafungwa wengine 200 hivi karibuni kukataa kula chakula wakilalamika dhidi ya kifungo kirefu bila ya kufikishwa mahakamani.Mjini Washington,msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani amesema kuwa wafungwa 252 wameondoshwa Guantanamo Bay tangu jela hiyo kufunguliwa January 2002 na kiasi ya 500 wengine bado wamezuiliwa huko.