1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUWAIT Mwanamke wa kwanza ateuliwa kuwa waziri

13 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4D

Waziri mkuu wa Kuwait, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Sabah, amemteua waziri wa kwanza mwanamke katika baraza lake la mawaziri. Shirika la habari la taifa limeripoti kwamba waziri mkuu huyo amemteua Massouma Mubarak kuwa waziri wa mipango na maswala ya maendeleo. Uteuzi huo umefanywa majuma machache baada ya Kuwait kuwapa wanawake haki ya kupiga kura.