1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya Kombe la Ulaya

Ramadhan Ali3 Desemba 2007

Timu 16 zitakazocheza finali ya Kombe la Ulaya Juni mwakani zajulikana.Itali,Ufaransa,Holland na Rumania kundi moja.

https://p.dw.com/p/CWHX
Bayern's Franck RiberyPicha: AP

Kura ilipigwa jumapili jinsi timu 16 za Ulaya zitakavyo pambana kwa kombe lijalo la Ulaya 2008.Lipi ni kundi gumu kabisa na la kufa-kupona ?

Kombe la Challenge Cup la Afrika mashariki na kati,laanza jumamosi hii ijayo nchini Tanzania wnyeji taifa Stars wakiwa na miadi na Harambee Stars (Kenya).

Mfaransa Franck Ribery,ameipeperusha Bayern Munich,kileleni tena mwa Bundesliga kwa bao lake la ushindi jana dhidi ya Armenia Bielefeld.

Katika kura ya kombe lijalo la Ulaya la mataifa jana mjini Lucerne,Uswisi,mabingwa wa dunia na makamo-bingwa Itali na Ufaransa zimeangukia kundi la kufa-kupona.Kwani,mbali na timu hizo 2 zilizocheza finali ya mwaka jana ya kombe la dunia hapa Ujerumani,kuna pia Holland na Rumania.

Kundi hili C ndilo gumu kabisa.Kocha wa Itali, Roberto Donadoni alisema alipata hisia hata kabla ya kura ya jana kwamba, mambo yangeenda hivyo.

Nae kocha wa Ufaransa Raymond Domenech,aliduwaa lakini alisema kundi hili linaahidi msisimko mkubwa.

Ujerumani,wamebahatika kidogo,kwani wameangukia kundi hafifu kidogo ukilinganisha na la wenazo wadachi,waazurri na wafaransa.

Ujerumani imeangukia kundi moja na wenyeji-Austria,Poland na Croatia.Ni Croatia,utakumbuka ikicheza na Sukar,ndio ilioichezesha Ujerumani kindumbwe-ndumbwe na kuipiga kumbo nje ya robo-finali ya kombe la dunia,1998 nchini Ufaransa.

Lakini, amelionaje kundi hili kocha wa Ujerumani Joachim Loew ?

“Nadhani Croatia,Poland na Austria mwenyeji,ni timu kali na si za kudharauliwa.Tuna nafasi nzuri hatahivyo,kucheza duru ijayo.”

Nae meneja wa timu ya taifa ya Ujerumani, Oliver Bierhof,alisema:

“Timu zote hizi zimestahiki kuwamo kwenye mashindano haya n a hata wenyeji Austria.Sijui vipi kukisia hali itakuaje,lakini ukiangalia kundi C lilivyo,unabidi kuridhika na kura ilivyotuangukia.”

Firimbi Italia jumamosi hii ijayo kuanzisha kinyan’ganyiro cha kombe la Afrika Mashariki na Kati.Wenyeji taifa Stars watafungua dimba na jirani zao Harambee Stars.Hili pengine litakua kombe la mwisho kuaniwa kituo kimoja-baadae mfumo utakua wa timu kucheza nyumbani na n’gambo-home and away- anaripoti mwanamichezo wetu George Njogopa:

Kutoka Tanzania,tuvuke sasa mpaka tukijiunga na eric Ponda mjini Mombasa,akitusimulia viwanja vya michezo vilikuaje mwishoni mwa wiki ?

Ligi maarufu za Ulaya zilitamba pia mwishoni mwa wiki:Katika Bundesliga,mfaransa Franck Ribery,alilifumania jana lango la Armenia Bielefeld kwa bao lake maridadi ajabu na kuirudisha Bayern Munich kileleni mwa ngazi ya Bundesliga.Hapo kabla Werder Bremen,ilitamba mbele ya Hamburg kwa mabao 2:1 na kuunyakua usukani wa Ligi kwa masaa 24.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza, Arsenal iliendeleza rekodi yake ya kutoshindwa hadi sasa msimu huu ilipoizaba Aston villa mabao 2-1.

Katika serie A,ligi ya Itali, Inter Milan wamefungua mwanya wa pointi 3 kileleni baada ya kuizaba Fiorentina mabao 2:0 mwishoni mwa wiki.As roma iko nafasi ya pili kufuatia ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi yaUdinese.Juventus wako nafasi ya 3.

Katika la Liga-Ligi ya Spian, Real Madrid iliochapwa mabao 3-2 na Bremen katika champions League hivi majuzi ilipanua uongozi wake kwa hadi pointi 4 baada ya kuishinda Racing Santander mabao 3-1.

Kaka, stadi wa Brazil,anaeichezea mabingwa wa Ulaya AC Milan,atunzwa taji la mwanasoka bora wa Ulaya-“Ballon d’Or.”

Na kwa zawadi hiyo aliostahiki Kaka,ndio sina budi bali kuishia hapo kwa leo.