Kombe la Dunia 2010 | Michezo | DW | 12.06.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la Dunia 2010

Argentina yiliongoza bao 1:0 kipindi cha kwanza dhidi ya Nigeria.

default

Tshabalala ashangiria bao lake langoni mwa Mexico jana.

Baada ya Korea ya kusini kuizaba Ugiriki ,mabao 2:0 katika siku ya pili ya Kombe la Dunia 2010,Nigeria na Argentina, zimerudi uwanjani kwa kipindi cha pili huko Elis Park,Stadium, Johannesberg. Vuvuzela zikihanikiza,

Argentina, ilitangulia kwa bao la kwanza mnamo dakika ya 6 ya mchezo na laiti si kipa Enyama wa nigeria alieokoa maridadi ajabu,Argentina ingekuwa 2:0 baada ya dakika 20 za mchezo. Obesi wa Nigeria anaecheza Bundesliga, alikuwa hatari mara 3 katika lango la Argentina. Argentina, iliongoza kwa bao 1:0 kipindi cha kwanza. Lioenl Messi pia alikosea baada ya kipa Enyama kuokoa.

KOMBE LA DUNIA NA VUVUZELA:

Kombe la Dunia 2010 la kwanza barani Afrika, lilianza kwa kishindo,shangwe na shamra shamra huko City Stadium mjini Johannesberg.Baada ya kuongoza kwa bao 1 hadi dakika ya 80 ya mchezo,Mexico iliwatilia Bafana Bafana kama walivyoahidi kitumbua chao mchanga na kuzima matarumbeta ya vuvuzuela .Kocha wa afrika kusini,Carlos parreira, aliwapa watoto wake wa Bafana Bafana leo Juammosi siku ya mapumzilo.Shabiki wa Mexico akibisha bao lao lililokataliwa na rifu kwa kuotea,alisema,

"Hakuotea,lakini daima rifu huwa wanaelemea timu ya nyumbani."

Hatahivyo, mashabiki wa Bafana bafana, waliridhika na sare ya bao 1:1 na wanasema:

"Unajua mambo ndio yamekwenda hivyo -ni pointi 1,lakini , tutarudi tu.Tumepungukiwa na pointi 3 na tutazichukua kwa wafaransa.

Wafaransa, chungeni tunakuja."

Shabiki mwengine wa afrika Kusini akasema,

"Tunapaswa kuishinda sasa Ufaransa na Uruguay na tutashinda-hakuna matata."

Baadae leo usiku,itakua zamu ya Uingereza, kupambana na Marekani.Je,Wayne rooney atatamba ?

Ujerumani, mabingwa mara 3 wa dunia, watakuwa uwanjani kesho usiku wakiwa na miadi na Kangaroo Australia.Wakiongoza na nahodha Philipp Lahm, chipukizi wa Ujerumani,watumai kunyakua pointi 3 za kwanza kabla mtihanmi wao mgumu Juni 23, watakapopambana na Black Stars-Ghana.

Ivory Coast na nahodha wao Didier Drogba,watakuwa uwanjani Jumaane wakipambana na Ureno na cristiano Ronaldo katika kundi G-kundi la kufa-kupona. Brazil, mabingwa mara 5 wa dunia, siku hiyo watafungua dimba na Korea ya Kaskazini kujaribu wao kuzima makombora yao ya nuklia.

Mwandishi: Ramadhan Ali /AFPE

Uhariri:Aboubakary Liongo