Kombe la dunia 2010 | Michezo | DW | 09.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kombe la dunia 2010

Uwanja wa mji wa Mandela Bay,huko Port Elizabeth hautachezewa kombe la mashirikisho mwakani.

Gharama za ujenzi wa viwanja vya kombe lijalo la dunia 2010 zimezidi kwa kima cha 33% na kufikia dala milioni 384 zaidi ilivyopangwa.

Mji wa Mandela Bay, nchini Afrika kusini, umekasirika kwa kufuatwa kuwa kituo cha kombe la mashirikisho hapo mwakani-kombe linalofungua pazia mwaka mmoja kabla kuanza kombe la dunia :

►◄

Kamati ya maandalio ya kombe lijalo la dunia ya mji wa Mandela Bay,Afrika Kusini imetangaza kuwa uwanja wa mji huo hautatumiwa tena kwa mashindano ya kombe la mashirikisho -confederations cup-kombe la timu bingwa za kitaifa na mwenyeji kutoka mabara yote.Sababu ni kuwa uwanja wa jiji hilo huko Port Elizabeth, hautaweza kumalizika kabla Machi 30 -muda wa mwisho uliowekwa .

Katika taarifa ilitoka jana ,naibu wa diwani wa jiji la Mandela Bay.Bicks Ndoni amesema manispaa ya jiji hilo yasikitishwa sana na uamuzi huo.

Akaongeza kuwa uwanja huo utakuwa tayari na kutimiza masharti yote ya FIFA ya kukamilisha hadi Machi 29,mwakani-mapema kabla kuanza kwa kombe la mashirikisho linalofungua pazia la kombe la dunia .Kombe hilo limepangwa Juni 14-28.

Ndoni aliarifu jana kwamba, sio ujenzi wa uwanja wa dimba unakwenda sawa sawa bali mipango yote tangu ya maandalio ya kombe la mashirikisho hata ya kombe la dunia yamefika mbali.

Mbali na kisa cha kufutwa kwa Nelson Mandela Bay city kama kituo cha Confederations cup, gharama za maandalio ya viwanja vya kombe la dunia kwa jumla zimezidi kwa kima cha 33& na kufikia dala milioni 384 zaidi kuliko ilivyopangwa awali.

kuongezeka huko kwa gharama kutapelekea matumizi ya ujnezi wa viwanja 5 vipya na kuvikarabati vyengine 5 kufikia Rand bilioni 13na hii ni kiasi mara mbili ya kima cha awali cha Rand bilioni 6.7 zilizokisiwa na serikali pale Afrika Kusini ilipogombea kuandaa kombe la dunia 2004.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalio ya kombe la dunia Jordaan amesema kamati yake ina hakika itapata fedha hizo zaidi.

Makamo wa waziri wa fedha wa Afrika Kusini, Jabu Moloketi ameliambia gazeti la City Press mwishoni mwa wiki kuwa miji 9 itayoandaa kombe la dunia itapaswa sio tu kutegemea serikali bali pia Banki ya Maendeleo ya Afrika kwa mikopo ya riba ndogo kujaza pengo la gharama zilizozidi.

Ughali wa maisha nchini Afrika kusini, umeongezeka kwa kima cha 10.9% hapo mei na kupindukia kima cha 3-6 % kilichokisiwa na serikali. Thamani ya Rand pia imeanguka mno mbele ya sarafu kubwa mnamo mwaka uliopita huku Afrika kusini ikijikuta katika msukosuko wa machafuko ya kisiasa.

Sarafu dhaifu ya rand inazidisha gharama ya vifaa vya ujenzi mfano wa paa kutoka Ujerumani la uwanja wa City Stadium nje ya jiji la Johannesberg.Ni katika uwanja huu ndiko mechi ya ufunguzi na finali ya kombe la dunia itakochezwa.