Kombe la Afrika la Mataifa laanza jumapili Accra. | Michezo | DW | 14.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la Afrika la Mataifa laanza jumapili Accra.

Sudan imeangukia kundi C pamoja na mabingwa Misri,Kamerun na zambia.nini hatima yake ?

default

Juergen Klinsmann na rais wa B.Munich K.Rummenige

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,Manchester united imeizaba Newcastle mabao 6-0 na kuunyakua usukani wa ligi hiyo wakati mahasimu wao Arsenal wamemudu suluhu tu ya bao 1:1 na Birmingham City.

Bundesliga ikiwa bado likizoni,viongozi wa ligi-Bayern Munich wametangaza kuwa stadi wa timu ya taifa na Werder Bremen Tim Borowski,atajiunga na Munich chini ya kocha wao mpya msimu ujao Jürgen Klinsmann.

kombe la Afrika la mataifa linapiga hodi jumapili ijayo pale Ghana na Guinea zitakapofungua dimba mjini Accra. Sudan-ndie muakilishi pekee wa CECAFA-shirikisho la dimba la Afrika mashariki na kati na mabingwa wao wa challenge Cup:

Mchezaji wa Taifa wa Ujerumani anaeichezea wakati huu Werder Bremen,Tim Borowski,atajiunga na Bayern Munich pale kocha wao mpya na mchezaji wao wa zamani Jürgen Klinsmann, atakapompokea mikoba kocha wa sasa Dietmar Hitzfeld.

Werder Bremen-klabu ya sasa ya Borowski ilitangaza jana kwamba Borowski alikataa kurefusha mkataba wake na ameamua kujiunga na Bayern Munich kucheza chini ya kocha mpya Klinsmann.Borowski akiwa na umri wa miaka 27 alikuwa mmoja wa timu ya Taifa ya Ujerumani iliomaliza nafasi ya tatu katika kombe la dunia 2006.Klinsmann ataanza kazi kama kocha mpya wa bayern munich hapo Julai 1.

Ligi ya Uingereza-premier League iliiona Manchester United mwishoni mwa wiki ikiparamia kileleni na kushjika usukani baada ya mahasmu wao Arsenal kuteleza na kutoka suluhu.

Manchester iliirarua New Castle kwa mabao 6 bila jibu wakati Arsenal iliondoka uwanjani sare bao 1:1 na Birmingham City.

Msukosuko huo wa kupoteza pointi 2 kwa Arsenal, ulimsikitisha sana kocha wao Erwin Senger.

„Mashabiki daima wakiiungamkono timu yetu ,lakini juu ya hivyo, hatukuingiwa na shime kuongeza kasi ya mchezo.

„Bila shaka, tumevunjwa moyo kwa sababu hatukucheza mchezo wetu bora kabisa hii leo na tumepoteza hapa pointi 2 muhimu sana.“

Alisema kocha wa Arsenal.

Katika la Liga-Ligi ya Spain ,Real Madrid iliomaliza kipindi cha kwanza cha msimu huu ikiwa na mwanya wa pointi 7 .Jana Real iliizaba Levante mabao 2:0

Kwanza Real ilinasa wavu kwa mkwaju wa penalty aliouchapa van Nistelrooy.

FC barcelona inayonyatia nafasi ya pili iligundua haijakosea kumbakisha jogoo la Kameroun,Samuel Eto’o mjini Barcelona na asitorokee Ghana kwa kombe la Afrika la mataifa kabla mchezo wa jumamosi.

Barcelona iliilaza Murcia huku Eto’o akitoa mchango mkubwa.

Wiki ijayo, simba wa nyika Kameroun itamtegemea Samuel Eto’0 kuongoza hujuma zao za kuwavuta taji Misri mabingwa wa sasa wa Afrika.

Akiwa nje ya chaki ya uwanja kwa miezi , Samuel Eto’o ameibuka kuwa mshambulizi hatari wa kutia mabao mnamo misimu 2 iliopita nchini Spain.

Kameroun imeanguikia kundi hafifu katika kombe la Afrika la mataifa –kundi C likijumuisha mabingwa Misri, mabingwa wa Afrika mashariki na kati Sudan na chipolopolo Zambia.

Samuel eto’0 ambae hapo okotoba alifuata nyayo ya Ronaldinho-mwenzake katika klabu ya Barcelona kuchukua uraia wa Spian pamoja na ule wa kameroun,atakua usoni kabisa mwa kikosi cha kocha mjerumani Otto Pfister kwa kombe lijalo la Afrika.

Tukibakia katika Kombe la Afrika la mataifa,Sudan waakilishi pekee wa kanda ya Cecafa ya Afgrika mashariki na kati nchini Ghana, wametangaza hivi punde kikosi chao cha wachezaji 23 kikitokana hasa na klabu zao 2-Al Hilal na Al Merreikh.Al Hilal imechangia wachezaji 12 wakati Al Merreikh ,waliosalia.

Kocha wa Sudan Mohammed Abdallah amemrejesha katika kikosi chake mshambulizi Feisal Agab,alieibuka mtiaji mabao mengi wakati Sudan ikiania tiketi ya finali hiozi za kombe la Afrika.

Kikosi cha Sudan kinajumuisha pia Abdelhamid Amari aliepata sifa nyingi alipotamba katika kikosi chake kilichotwaa kombe la Challenge Cup mwezi uliopita nchini Tanzania pale Sudan ilipoipiga kumbo Ruanda na kotoroka na kombe.

Hii ni mara ya kwanza tangu kupita miaka 32, sudan,muasisi wa kombe la afrika la mataifa nyumbani Khartoum, 1957 inashiriki tena katika finali za kombe hili.

Sudan itacheza mchezo wake wa kwanza hapo jumaane ijayo mjini Kumasi ikipambana na chipolopolo-Zambia.Ukichukulia hizi ni timu 2 pekee hafifu katika kundi hili lenye kuingiza mabingwa Misri na simba wa nyika –Kameroun, Sudan itapaswa kujiwinda barabara kujikinga na risasi kali za chipolopolo.