KHARTOUM: Mjumbe wa Umoja wa Ulaya kubakia Sudan
25 Agosti 2007Matangazo
Sudan itamruhusu mjumbe wa Umoja wa Ulaya aliefukzwa siku ya Alkhamisi,kubakia nchini Sudan hadi mwezi ujao,ambapo muda wa wadhifa wake utamalizika.
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan, ilimfukuza balozi wa Umoja wa Ulaya Kent Degerfelt pamoja na mwanadiplomasia wa Kanada,Nuala Lawlor kwa sababu ya kuhusika na harakati ambazo Sudan imesema,ni kuingilia mambo yake ya ndani.