KABUL: Washukiwa wa utekaji nyara wakamatwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Washukiwa wa utekaji nyara wakamatwa

Polisi nchini Afghanistan wamewatia mbaroni watu wanne wanaoshukiwa kumteka nyara mwanamke wa kijerumani aliyeachiwa huru usiku wa kuamkia leo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan amesema leo mjini Kabul kwamba washukiwa wote wanne, akiwemo kiongozi aliyepanga njama ya kumteka nyara mjerukani huyo, walikamatwa wakati wa harakati za kumuokoa mateka huyo.

Mwanamke huyo aliachiliwa huru kufuatia operesheni iliyoandaliwa na wizara ya mambo ya ndani na shirika la ujasusi la Afghanistan iliyowajumulisha maafisa 300 wa usalama.

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani mjini Berlin imethibitisha kuachiwa huru Christiana Meier aliyetekwa nyara juzi Jumamosi na wanaume wanne wakati alipokuwa akiondoka mgahawa mmoja magharibi mwa mji mkuu, Kabul akiwa na mume wake.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com