KABUL: Shambulizi la bomu lamwaga damu Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 29.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Shambulizi la bomu lamwaga damu Afghanistan

Mshambulizi aliejiripua na bomu ndani ya basi katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul ameua watu 27 na kujeruhi 29.Wengi waliouawa walikuwa wanajeshi.Idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwa sababu majeruhi 17 ni mahututi.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya ulinzi,basi hilo lilikuwa likisafirisha wanajeshi kazini,mtu alievaa sare ya kijeshi alipolikaribia na kujiripua.Waasi wa Taliban wamedai kuhusika na shambulizi hilo na kuongezea kuwa ni sehemu ya operesheni walioanzisha majuma mawili yaliyopita dhidi ya vikosi vya serikali na vya kimataifa nchini Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com