KABUL: Mwanajeshi wa ISAF ameuawa Afghanistan
19 Agosti 2007Matangazo
Mwanajeshi mmoja wa vikosi vya kimataifa vinavyolinda usalama nchini Afghanistan,ISAF ameuawa katika shambulizi la bomu,kusini mwa nchi.Kwa mujibu wa afisa wa ISAF katika mji mkuu Kabul,mwanajeshi huyo alikuwa akiusindikiza msafara wa magari ya kijeshi.Afisa huyo lakini hakueleza uraia wa mwanajeshi alieuawa.