Jukwaa la Al Jazeera | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Jukwaa la Al Jazeera

Kituo cha TV cha kiarabu "Al jazeera" sio kituo cha kigaidi bali ni mtetezi wa uhuru wa habari.

“Nakiungamkono kituo cha TV cha Al Jazeera kwa sababu kimetenda zaidi kueneza demokrasia katika mashariki ya kati kuliko mtu yeyote na bila ya shaka zaidi ya serikali ya marekani .”

Bingwa wa vyombo vya habari Hugh Miles ameliambia shirika la habari la IPS.

Miles alizungumza na shirika la IPS katika jukwaa la kila mwaka la kituo cha TV cha Al Jazeera huko Doha ,nchini Qatar-jukwaa lililofanyika kati ya Machi 31 na juzi April 2.

Jukwaa hilo lilimurika kupanuka karibuni kwa chombo hicho cha habari wakati pia likielezea shida maripta wanazokabiliana nazo katika mashariki ya kati.

Miles muandishi wa makala chini ya kichwa ‘Al Jazeera:Jinsi gain kituo cha habari cha TV cha kiarabu kilivyotoa changamoto kwa dunia na muandishi habari wa reja-reja alietunzwa zwadi,alisema waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld,amekosea kukieleza kituo cha Tv cha Al Jazee ni kituo cha kigaidi.”terrorist network.”.Au kukiita ‘sauti ya osama’.Miles akasema hii yaonesha kutojua kwake kabisa historia na kituo hiki.

Kituo cha TV cha Al Jazeera chenye umri wa miaka 10 sasa tangu kuasisiwa, kilipambana na hujuma za majeshi ya Marekani katika afisi zake mjini Baghdad wakati Marekani ilioongoza uvamizi nchini Irak April,2003.

Kikakabiliwa na mashtaka na tuhuma kutoka kwa Rumsfeld kwamba kikipalilia ugaidi kwa kuonesha picha kama zile zan unyongaji na kukatwa watu vichwa.

Waandishi habari wa Al jazeera wanasema hawakuwahi kuonesha picha za kukatwa watu vichwa wala hakiungimkono ugaidi.

Wasemaji wengine katika jukwaa hilo walikiiungamkono na kukipongeza kituo cha Al Jazeera ambacho kikihujumiwa kwa aina mbali mbali na wakereketwa wake.

Jukwaa hili mjini Doha liliwakusanya pamoja waandishi habari,viongozi wa vyombo vya habari vya kimataifa, na wasomi kutoka kila pembe ya dunia.Walitwa kujadiliana maswali muhimu kabisa yanayovikabili vyombo vya habari hii leo.

Abdul Bari Atwan,mhariri-mkuu wa gazeti la kiarabu al –Quds lenye kituo chake mjini London, aliliambia shirika la IPS kwamba waandishi habari wapaswa kuungana pamoja kupaza sauti moja kupinga wanavyotendewa na viongozi wa dola zinazojiita za ulimwengu huru,watu wanaokandamiza uhuru wa kujieleza.Tuungane-aliongeza Abdul Bari kupinga mfumo wa uandishi habari wa kuongozana na wale wanaotenda mambo-embedded journalism,kwani mtindo kama huo ni uchujaji wa habari.

“Uhuru wa kujieleza unasemekana ni sehemu ya maadili ya nchi za magharibi.”-aliongeza Abdu Bari Atwan.”Utawala wa Marekani unateketeza maadili ya kimagharibi kwa kuwafyatulia riasi waandishi habari ,kwa kumuua mjumbe-wakati mjumbe hauwawi-asema Abdul Bari.

Wauaji wakubwa wa waandishi habari ni serikali-alisema Frank s myth-mjumbe mjini Washington wa Kamati ya kuwalinda waandishi habari (CPJ).

Waandishi habari wengine watiwa kizizini bila ya hata kufunguliwa mashtaka.Kwa mfano, mpigakamera wa Al jazeera, Sami al-Hajj,msudani,aaliwekwa kizizini na Jeshi la Marekani, nchini Afghanistan hapo Desemba 2001.Bado hata kufunguliwa mashtaka na yungali akiangaliwa kama ni mpiganaji adui katika Gereza la Guantanamo.

Jukwaa hili huko Doha,Gatar- nyumbani mwa Al Jazeera,lilizungumzia mada mbali mbali mfano ‘uandishi habari wenye kina” au uandishi habari wa “kuchupia-chupia” tu.

Lakini mada kuu ilibaki kuwa hujuma dhidi ya waandishi habari katika hali inayozidi kutatanisha ulimwenguni.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com