Juhudi zaidi za kutaka kuachiwa mwalimu wa Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 03.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Juhudi zaidi za kutaka kuachiwa mwalimu wa Uingereza

KHATOUM.Wanasiasa wawili waislam wa Uingereza asubuhi wanakutana na Rais Omar Hassan al Bashir katika juhudi za kutaka kuachiwa huru kwa mwalimu mmoja wa Uingereza.

Wanasiasa hao Baroness Warsi ambaye ni mwanamke kutoka chama cha Conservative na Lord Ahmed kutoka Labour wamesema kuwa pamoja na ugumu uliyopo katika majadiliano lakini wana matumaini ya kufikiwa muafaka suala hilo

Mwalimu huyo Gillian Gibbons wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha siku 15 na mahakama ya Sudan baada ya kuwaruhusu wanafunzi wake kumpachika jina sanamu ya dubwi jina la mtume Muhammad SAW.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com