1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Rice auwekea matumaini mkutano wa amani

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Er

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice amekamilisha ziara yake ya siku nne Mashariki ya Kati kwa kusema kwamba mkutano unaokuja wa amani ya Mashariki ya Kati una nafasi kubwa ya kufanikiwa.

Hata hivyo Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina amemtahadharisha Rice kwamba Wapalestina wanaweza kutoshiriki mkutano huo iwapo mazungumzo ya hivi sasa na Israel hayatopiga hatua ya kuridhisha.Abbas anataka kwenda kwenye mkutano huo uliopangwa kufanyika Annapolis nchini Marekani hapo mwezi wa Novemba akiwa na waraka wenye ufafanuzi wa kina juu ya masuala nyeti yanayohusu mzozo wa Israel na Wapalestina.

Israel imeukataa wito huo wa Abbas ikiwa ni pamoja na suala la kuweka ratiba maalum ya utekelezaji wa maafikiano yao.