JERUSALEM: Duru ya pili kuchagua kiongozi wa Labour
12 Juni 2007Matangazo
Chama cha Labour nchini Israel,kinapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi ambao huenda ukaamua hatima ya Waziri Mkuu Ehud Olmert.Katika duru hii,waziri mkuu wa zamani Ehud Barak anapambana na aliekuwa mkuu wa upelelezi,Ami Ayalon ambae ni mgeni katika uwanja wa kisiasa. Wagombea hao wawili,wamedokezea kuwa watakitoa chama cha Labour kutoka serikali ya mseto pamoja na chama cha Kadima,ikiwa Ehud Olmert hatongatuka madarakani.