JERUSALEM: Barak ateuliwa kama waziri mpya wa ulinzi
16 Juni 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert amemteua, kiongozi wa chama cha Labour aliechaguliwa hivi karibuni,kuwa waziri wake mpya wa ulinzi.Ehud Barak,anachukua nafasi ya Amir Peretz aliekuwa kiongozi wa chama cha Labour kabla ya kushindwa na Barak mapema juma hili.Uteuzi wa Barak kama waziri wa ulinzi,unatarajiwa kuidhinishwa rasmi bungeni,siku ya Jumatatu.Wakati wa kampeni za uchaguzi kuwania uongozi wa chama cha Labour, Barak alitoa wito kwa Ehud Olmert kuondoka madarakani kwa sababu ya jinsi vita vya msimu wa kiangazi uliopita vilivyoendeshwa,dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.