Islamabad.Mchunguzi wa Kifaransa aonya hatari endapo Iraq itagawika kikabila. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Islamabad.Mchunguzi wa Kifaransa aonya hatari endapo Iraq itagawika kikabila.

Kwa mujibu kiongozi wa ngazi ya juu wa shirika la Kifaransa linaloshughulikia masuala mbali mbali nchini Iraq amesema, kuitenganisha kikabila nchi hiyo ni sawa na kuivuruga Mashariki ya Kati nzima na athari zake pia zinaweza kuenea nchini Pakistan na Afghanistan.

Akinukuliwa na gazeti la Pakistan “Daily Taimes“ mchunguzi huyo amesema, Pakistan inaweza ikaathirika ikiwa Iraq itatenganishwa kikabili, na baada ya hapo athari hizo zitasambaa katika maeneo mengine ya huko Baluchistan.

Ameongeza kuwa, mgawanyiko wa Iraq utaiathiri zaidi Uturuki ambako Wakurdi waliojitenga wanapigana na Ankara kutaka taifa huru la Kikurdi ambalo Wakurdi wa nchini Iraq nao watataka kujiunga nalo.

Aidha mchunguzi huyo kutoka Ufaransa ameionya Marekani dhidi ya kuishambulia Iran kwa kusema kuwa, Marekani itakula hasara kwa pande zote mbili nchini Iraq na Afghanistan ikiwa Rais Bush ataamuru majeshi kuizuia Tehran isitengeneze Bomu la Kinyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com