ISLAMABAD : Waziri wa ulinzi wa Taliban mbaroni | Habari za Ulimwengu | DW | 03.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Waziri wa ulinzi wa Taliban mbaroni

Pakistan inasema vikosi vyake vya usalama vimemkamata waziri wa zamani wa ulinzi wa kundi la Taliban Mullah Obaidullah Akhund ambaye anaonekana kuwa ni kiongozi mwandamizi kabisa anayeshikilia nafasi ya tatu katika kundi hilo la itikadi kali.

Akhund inaripotiwa kuwa ni miongoni mwa watuhumiwa watano wa Taliban waliokamatwa wakati wa msako kwenye nyumba kusini magharibi mwa mji wa Quetta nchini Pakistan mapema wiki hii.Taliban imezikanusha taarifa hizo.

Akhund inaaminika kuwa ni mshirika mkuu wa kiongozi wa Taliban anayesakwa Mula Omar na anakuwa kiongozi mwandamizi kabisa kutoka kundi hilo la wanamgambo wa itikadi kali za Kiislam kutiwa nguvuni tokea kupinduliwa kwake madarakani nchini Afghanistan zaidi ya miaka mitano iliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com