Iran yasema "haina imani" na Marekani kwenye mazungumzo
15 Mei 2026
Matangazo
Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araghchi pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mataifa yanayounda kundi la BRICS unaofanyika kwenye mji mkuu wa India, New Delhi.
Ama kuhusu suala la kufungwa kwa Ujia wa Bahari wa Hormuz mwanadiplomasia huyo wa Iran, amesema, "Kwa tunavyofahamu, Mlango Bahari wa Hormuz uko wazi, na meli zote zinapita isipokuwa meli zinazomilikiwa na nchi zilizo kwenye vita na sisi, zile zinazopigana nasi"
Marekani na Iran zilitangaza kusitisha vita kwa muda mwezi uliopita lakini hadi sasa zimeshindwa kufikia makubaliano ya kudumu ya amani licha ya juhudi nzito za kidiplomasia zinazoongozwa na Pakistan.