HYDERABAD: Mripuko wa bomu msikitini umeua 14 | Habari za Ulimwengu | DW | 19.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HYDERABAD: Mripuko wa bomu msikitini umeua 14

Watu 14 wameuawa kusini mwa India baada ya bomu kuripuka katika msikiti wa kihistoria mjini Hyderabad.Si chini ya watu 50 vile vile walijeruhiwa katika mripuko huo wa bomu.Polisi wamesema,wamefaulu kuzuia mabomu mengine mawili kuripuka,baada ya kugundiliwa katika msikiti huo wa kale katika mji wa Hyderabad.Mapambano pia yalizuka kati ya polisi na umati wenye hasira uliokusanyika kufuatia mripuko huo wa bomu.Waziri Mkuu wa jimbo la Andhra Pradesh,ambalo mji wake mkuu ni Hyderabad,ametoa wito kwa wakazi wa madhehebu za Kihindu na Kiislamu kubakia shuari, ikihofiwa kuwa shambulio hilo la bomu msikitini, huenda likazusha machafuko kati ya jamii hizo mbili.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com