Harare. Viongozi wa upinzani wakamatwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Harare. Viongozi wa upinzani wakamatwa.

Nchini Zimbabwe, polisi wa kuzuwia ghasia wamewakamata viongozi wa ngazi ya juu wa upinzani nchini humo. Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change, alilazimishwa kusimamisha gari lake na polisi pamoja na maafisa wengine wa upinzani wakati wakisafiri kuelekea katika mkutano wa upinzani dhidi ya serikali mjini Harare.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa mtu mmoja alipigwa risasi na kufa na polisi hao, katika mvutano unaohusiana na suala hilo.

Hali ya wasi wasi wa kisiasa imepanda nchini Zimbabwe wakati nchi hiyo ikitumbukia zaidi katika mzozo wake wa kisiasa kwa miongo kadha, wakati ughali wa maisha umepanda na kufikia asilimia 1,700, ukosefu wa nafasi za kazi ukiwa katika asilimia 80 na ukosefu jumla wa chakula na petroli ukiongezeka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com