HANOI: Korea ya Kaskazini yahimizwa kuachulia mbali mradi wa kinuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI: Korea ya Kaskazini yahimizwa kuachulia mbali mradi wa kinuklia

Mkutano wa nchi 21 zinazoshirikiana kiuchumi katika eneo la Asia na Pacifik-APEC umetoa mwito kwa Korea ya Kaskazini kusitisha mpango wake wa kutengeneza silaha za kinuklia.Katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano wa kilele wa APEC nchini Vietnam,viongozi wa nchi na serikali wameeleza wasi wasi wao kuhusu jaribio la kinuklia lililofanywa na Korea ya Kaskazini mwezi wa Oktoba.Serikali ya kikomunisti ya Pyongyang, imehimizwa kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa na kurejea kwenye meza ya majadiliano.Mbali na mada ya kinuklia ya Korea ya Kaskazini,mkutano wa Hanoi hasa ulishughulikia masuala ya kiuchumi. Madola ya APEC,yamesisitiza kwamba majadiliano mapya yanapaswa kufanywa kuhusika na suala la kupunguza ruzuku.Nchi hizo vile vile zimeamua kushirikiana zaidi kupiga vita ulaji rushwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com