GAZA:Israel yakubali kuwapokea wakimbizi wa vita kutoka Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 20.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Israel yakubali kuwapokea wakimbizi wa vita kutoka Gaza

Mapambano makali kati ya wanamgambo na wanajeshi wa Israel yanaendelea huko Gaza.

Opresheni hiyo imesababisha watu kukimbia makaazi yao kwenye eneo hilo.Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak ametoa amri kwa wanajeshi kuruhusu wapalestina wanaohitaji huduma ya matibabu kuingia Israel. Kiasi cha wapalestina 200 wengi wakiwa wagonjwa na waliojeruhiwa wamekwama kwa muda wa wiki moja katika kivuko cha Erez cha kuingia upande wa Israel kutoka ukanda wa Gaza.

Wanajeshi wa Israel wamewauwa wanamgambo wanne wakipalestina katika mapambano mabaya kabisa kuwahi kutokea tangu kundi la Hamas kudhibiti eneo hilo wiki iliyopita.

Katika tukio jingine tofauti karibuni na mji wa Jenin Ukingo wa Magharibi wanamgambo wengine wawili wakipalestina waliuwawa katika mapambano ya risasi na wanajeshi wa Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com