GAZA: Wapalestina wanne wauwawa katika Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wapalestina wanne wauwawa katika Ukanda wa Gaza

Wapalestina wanne wameuwawa leo katika shambulio la jeshi la Israel dhidi ya wanamgambo wa kipalestina katika ukanda wa Gaza.

Kwa mara ya kwanza tangu Israel ilipoondoka Gaza, majeshi ya Israel, yamesonga katika eneo la mpakani kati ya Misri na Gaza.

Duru zinasema wanamgambo wawili wa kipalestina wameuwawa wakati wanajshi wa Israel walipoingia katika mji wa Rafah mapema leo.

Jeshi la Israel limesema operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi ya kutafuta mahandaki yanayotumiwa na wanamgambo wa kipalestina kuingiza silaha kutoka Misri.

Maofisa wa Palestina wamesema majeshi ya Israel yamefanya msako wa nyumba kwa nyumba na wametumia matingatinga kuharibu mashamba yaliyo karibu na mpakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com