GAZA: Wapalestina 7 wauawa ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wapalestina 7 wauawa ukanda wa Gaza

Kwa uchache Wapalestina 7 wameuawa na wengine 14 wamejeruhiwa wakati majeshi ya Israeli yakiingia katika ukanda wa Gaza. Jeshi la Israeli limesema wamevizia wapiganaji wa kipalestina waliokuwa wakilenga kurusha makombora kuelekea kusini mwa Israeli. Katika tukio jingine, kwa uchache Wapalestina 4 wameuawa katika ulishianaji risase kwenye ukanda wa Gaza ambapo wakaazi wanawalaumu wanajeshi wa Israeli kuhusika. Lakini duru za idara za usalama za wapalestina zinasema inawezekana yalikuwa mapigano kati ya familia adui.

Mbali na hayo, askari jeshi wa ulinzi wa rais Mahmud Abbas aliuawa jana katika tukio la risase na wapiganaji wa chama cha Hamas kwenye ukanda wa Gaza, siku mbili baada ya msafara wa gari zilizokuwa zikimsafirisha waziri mkuu Isamail Haniya kushambuliwa na watu wenye silaha.

Mkesha wa tukio hilo, waziri mkuu wa Palestina, Ismail Haniya, alitoa mwito wa kuweko umoja wa kitaifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com