GAZA: Wafanyakazi wawili wa Msalaba mwekundu watekwa nyara Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 22.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wafanyakazi wawili wa Msalaba mwekundu watekwa nyara Gaza

Watu waliokuwa na silaha wamewateka nyara wafanyakazi wawili wa misaada kwenye ukanda wa Gaza. Maafisa wa Palestina wamesema watu hao wawili waliotekwa nyara ni wafanyakazi wa shirika la Msalaba mwekundu na kwamba wamekamatwa katika mtaa wa Deir el-Balah kati kati mwa jiji la Gaza.

Kwa upande mwingine wapalestina 11 wamejeruhiwa katika shambulio la ndege za Israeli kwenye mji wa Beit Hanun kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, katika kile kimekumbusha mashambulizi ya hivi karibuni ya Israeli ambayo yalisababisha mauaji ya raia wa kipalestina 19.

Jeshi la Israel limesema mji huo wa Beit Hanun umekuwa ukitumiwa na wapiganaji wa kipalestina kushambulia kwa makombora nchini Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com