GAZA: Maofisa wa usalama waandamana | Habari za Ulimwengu | DW | 21.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Maofisa wa usalama waandamana

Maofisa wa vikosi vya usalama nchini Palestina leo wamefyatua risasi angani mjini Gaza na kuchoma matairi karibu na makaazi ya rais Mahmoud Abbas.

Maofisa hao walikuwa wakidai mishahara yao huku sikukuu ya Eid ul Fitri akikaribia katika eneo hilo. Moshi mweusi ulitanda katika anga ya mji wa Gaza huku maofisa hao wakiyazuia magari yasiingie mjini humo.

Wakati huo huo, wanajeshi wa Israel leo wamempiga risasi na kumuua mwanamume mmoja wa kipalestina mwenye umri wa miaka 50, kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati walipokuwa wakifanya operesheni yao ya kusaka mahandaki yanayotumiwa na wanamgambo kuingiza silaha kutoka Misiri.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com