GAZA CITY;:Mapigano makali yazuka tena ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY;:Mapigano makali yazuka tena ukanda wa Gaza

Mapigano mapya yamezuka leo hii kati ya vikosi vya polisi vya Hamas katika ukanda wa Gaza na ukoo wenye nguvu unaoegemea upande wa chama cha Fatah.

Duru za hospitali katika eneo hilo zimearifu kwamba kiasi cha watu wawili wameuwawa na kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Mapigano hayo yalizuka baada ya watu wa ukoo huo kulimiminia risasi gari lilikuwa limewabeba wapiganaji wa Hamas.Mapigano kama hayo yalizuka pia siku ya jumatano kati ya ukoo huo wa Hellis na askari wa Hamas ambapo watu wanne waliuwawa na wengine 30 wakajeruhiwa.

Mapigano ya jumatano ndiyo mabaya kabisa kuwahi kutokea tangu Hamas lilipochukua madaraka katika ukanda wa Gaza.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com