GAZA CITY : Kiongozi wa kidini auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Kiongozi wa kidini auwawa

Kiongozi wa kidini wa Gaza ambaye anafahamika vyema kwa maoni yake dhidi ya kundi la Hamas ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa kwenye gari wakati akitoka msikitini hapo jana.

Bado haijulikani nani waliohusika na mauaji hayo ya Adel Nasar ambayo yametokea wakati maelfu ya Wapalestina wakishiriki maandamano ya maziko huko Gaza ya kamanda wa usalama na walinzi wake sita wa kundi la Fatah la Rais Mahmoud Abbas wa Palestina.

Katika mkutano wa dharura mapema hapo jana Abbas na Waziri Mkuu wa Palestina Ismail Haniyeh wa kundi hasimu la Hamas linaloongoza serikali ya Palestin wametowa wito wa kukomeshwa kwa mapigano baina ya makundi hayo na kukubaliana kuondowa wapiganaji wao kutoka mitaani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com