FREETOWN:Uchaguzi wa kihistoria wafanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 12.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FREETOWN:Uchaguzi wa kihistoria wafanyika

Nchi ya Sierra Leone ilifanya uchaguzi wake wa kwanza hapo jana tangu majeshi ya kulinda amani kuondoka miaka miwili iliyopita.Uchaguzi huo wa kihistoria unatarajiwa kudumisha amani nchini humo baada ya kuzongwa na mapinduzi ya serikali vilevile vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu na kusababishwa na almasi.Wapiga kura waliwasili kabla alfajiri kwenye vituo vya kupiga kura ili kuteua kiongozi kati ya wagombea 7.Said Msonda msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Freetown anaeleza namna uchaguzi ulivyofanyika.

GO TO AUDIO

SIERRA LEONE O TON

Kwa mujibu wa maafisa wa tume ya uchaguzi shughuli ya kupiga kura ilifanyika vizuri bila visa vyovyote vya ghasia kuripotiwa.Changamoto kubwa kwa serikali mpya ni matatizo ya rushwa,umaskini na ukosefu wa nafasi za kazi mambo yaliyosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 10 na kumalizika mwaka 2002.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com